
Takehiro Tomiyasu - Beki wa Klabu ya Arsenal
Mjapani huyo mweneye umri wa miaka 26 alijiunga na Arsenal 2021 , msimu uliopita alicheza mechi 30 katika kikosi cha Mikel Arteta wakati msimu huu amecheza dakika 6 pekee dhidi ya Southampton mwezi Oktoba kutokana na kuandamwa na majeraha
"Nimefanyiwa upasuaji kwenye goti , imekuwa kipindi kigumu zaidi katika kazi yangu lakini sitakata tamaa,” ameandika Tomiyasu
Tomiyasu ataungana na winga wa Klabu ya Manchester United Amad Diallo ambaye pia alipata majeraha katikati yamsimu na kulazimuka kukaa nje hadi mwishoni mwa msimu huu