Shamaba la bangi likiteketezwa
Akiongea mara baada ya operesheni hiyo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo Aretas Lyimo amesema operesheni hiyo ni hatua kubwa ya vita dhidi ya dawa za kulevya.
"Hii ni operesheni kubwa ya kwanza kufanyika mkoani Dodoma, ikionyesha wazi kuwa kilimo cha bangi kimeanza kuenea katika baadhi ya maeneo ya mkoa huu tutaendelea kuchukua hatua kali kuhakikisha kuwa uzalishaji, biashara na matumizi ya dawa za kulevya vinadhibitiwa kwa nguvu zote," amesema Aretas Lyimo Kamishna DCEA.
Aidha Lyimo amesema katika kipindi cha Januari hadi Februari 2025 wamefanikiwa kukamata kilogramu 790.5 za aina mbalimbali ya dawa za kulevya pamoja na watuhumiwa 114 kwa tuhuma za biashara hiyo haramu.