
Mtoto mmoja na watu wazima wawili wamejeruhiwa vibaya katika ajali ya ndege iliyokuwa inatua katika uwanja wa ndege wa Toronto Pearson nchini Canada.
Mamlaka za uwanja wa ndege wa Toronto Pearson zilisema ajali hiyo ilihusisha ndege ya Delta Air Lines 4819 iliyokuwa ikitoka Minneapolis, na kwamba "abiria wote na wafanyakazi wa ndege wamepatikana."
Ndege hiyo ilikuwa na watu 80, wakiwemo abiria 76 na wafanyakazi wa ndege wanne, kama ilivyotangazwa na Delta. Abiria 22 kati yao ni Wacanada, wengine ni wa mataifa mbalimbali, alisema Ms. Flint.
Majeruhi 18 wamepelekwa hospitali, kwa mujibu wa Shirika hilo.Miongoni mwao, waliojeruhiwa vibaya ni pamoja na mtoto mmoja, mwanamume wa miaka 60, na mwanamke wa miaka 40. Abiria 22 kati yao ni Wacanada.