
Pep Guardiola - Kocha wa Manchester City na Earling Haaland
City wanakwenda Santiago Bernabeu wakitoka kushinda 4-0 dhidi ya Newcastle United. Ikumbukwe mchezo wa mkondo wa kwanza Man City walipoteza 3-2 katika Uwanja wa nyumbani ya wiki jana.
"Upeo wa kushinda Bernabeu katika nafasi hiyo, kila mtu anajua kwamba ukiniuliza kabla ya mchezo, asilimia ya kushinda na kupita, sijui ila tunafika 1%," Guardiola amesema.
Katika michezo 10 ya mwisho timu hizi kukutana Manchester City wameshinda michezo 5 huku Real Madrid wakishinda michezo 3 na kutoa sare katika michezo 2.