Monday , 17th Feb , 2025

Kocha wa Manchester United  Ruben Amorim amesema kibarua chake ni 'kigumu sana' baada ya kufungwa katika mchezo wa jana 1-0 dhidi ya  Tottenham 

Ruben Amorim Kocha wa Manchester United

Bao la James Maddison kipindi cha kwanza liliifanya Tottenham kupata ushindi wa kwanza kwenye uwanja wake wa nyumbani katika mechi nane za ligi kuu na kuwaacha Man Utd wakiwa katika nafasi ya 15 katika msimamo wa EPL

Mashetani wekundu wameshinda mechi 8 pekee katika michezo 25 walizocheza huku Ruben Amorim akishinda mechi 4 kati ya 14 tangu akabidhiwe timu hiyo kutoka mikononi mwa Ten Hag.

Tangu Amorim awasili United amefanya usajili wa beki Patric Dorgu katika dirisha ndogo la Januari huku akiwaruhusu Marcus Rashford na Antony kuondoka klabuni hapo kwa mkopo.