Monday , 17th Feb , 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi wa tuzo za wachekeshaji Tanzania 'Tanzania Comedy Awards' siku ya February 22,2025 ukumbi wa The Super Dome Masaki Dar es Salaam.

Picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan

Taarifa hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mwana FA katika tukio la All-Star Comedy Festival, lilofanyika Mlimani City.

Baadhi ya mastaa wa uchekeshaji waliotokea All Star Comedy Festival ni Coy Mzungu, Leonardo, Ndaro, Shafii Brand,SaidSaid, Kipotoshi, Nanga OG, Masantula na Eliud.