Saturday , 15th Feb , 2025

Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Ulaya (EU) zimeelezea kushtushwa na hali inayoendelea kuzorota katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya demokrasia ya Congo, na kutoa onyo dhidi ya hali ya mgogoro na ukiukaji wa uhuru wa kisheria wa nchi hiyo.

Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres, ameagiza majadiliano katika mkutano wa Umoja wa Afrika, saa chache baada ya vikosi vya waasi kudhibiti eneo zaidi katika jimbo la Kivu Kusini, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Bukavu.

Waasi wa M23 wanaendeleza mapigano mashariki mwa Congo, huku kukiwa na hofu ya kuenea kwa mgogoro huu katika eneo zima.

Bwana Guterres ameonya kwamba hakuna suluhu ya kijeshi na anatoa wito wa mazungumzo ya dharura kwa kupitia juhudi za upatanishi za kikanda.

Rais wa Congo, Félix Tshisekedi, ambaye hakuhudhuria mkutano wa AU huko Ethiopia, ameituhumu Rwanda kwa kuonyesha dhamira ya kutaka kupanua mipaka na ametoa wito wa vikwazo vya kimataifa dhidi ya Kigali.

Aidha anatoa wito kwa vyombo vya michezo vya kimataifa, ikiwa ni pamoja na NBA, Formula One, na vilabu vikubwa vya soka vya Ulaya, kusitishamikataba ya udhamini na Rwanda kadri mgogoro unavyozidi kuathiri maelfu ya watu na kuwalazimu kukimbia makazi yao