Thursday , 13th Feb , 2025

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linawashikilia watuhumiwa wawili ambao ni John Peter (45) dereva na mkazi wa Manyire Wilayani Arumeru Mkoani Arusha na Jafari Shirima (62) dereva na Mkazi wa Singida kwa kusababisha ajali iliyopelekea kifo cha Lucy John (40) mkazi wa Manyire.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo amesema kuwa Katika tukio hilo lililotokea tarehe 12.02.2025 muda wa 08:00 usiku huko maeneo ya Nganana barabara ya Afrika Mashariki mtuhumiwa John Peter aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T 499 CRR aina ya Noah aligonga kwa nyuma gari lilokuwa limeegeshwa barabarani lenye namba za usajili T 629 CLB aina ya Scania ikiwa na tela lenye namba za usajili T 447 BSL likiwa na dereva aitwae Jafari Shirima na kusababisha kifo cha Lucy John ambaye alikuwa abiria katika garia aina ya Toyata Noah.

SACP Masejo amefafanua kuwa mara baada ya kugonga gari hilo kwa nyuma mtuhumiwa John Peter alimshambulia dereva Jafari Shirima na kitu chenye ncha kali na kumsababishia majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake.

Aidha amebainisha kuwa Majeruhi anaendelea kupatiwa matibabu na mwili wa marehemu umehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi wa kitaaalam.

Kamanda Masejo akisistiza kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linatoa wito kwa kwa madereva kufuata sheria za usalama barabarabni ili kuepuka ajali. Pia tunatoa wito kwa watu  kuacha tabia ya kujichukulia sheria