Wednesday , 12th Feb , 2025

Mhitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Nyanza iliyopo mkoani Geita Rabia Paulo(19), amefariki dunia baada ya kujinyonga kutokana na msongo wa mawazo uliompata baada ya baraza la mitihani Tanzania kutangaza matokeo ya kidato cha nne na kukuta amepata daraja sifuri.

Mzazi wa Rabia

Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita SACP Safia Jongo amesema tukio hilo limetokea Februari 11, 2025, majira ya saa 10:00 jioni ambapo mwili wake umekutwa ndani ya chumba alichokuwa akiishi.

Jeshi la Polisi mkoani Geita limetoa wito kwa jamii kuwa na hofu ya mungu na kuzifahamu njia za kudhibiti msongo wa mawazo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza

Ambapo tayari mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitaalamu na kukabidhiwa kwa ndugu kwaajili ya taratibu za maziko.