Friday , 7th Feb , 2025

Dereva bodaboda anayefahamika kwa jina la Dickson Chacha(24), aliyekuwa mkazi wa Mtaa wa Machimbo kata ya Kipunguni jijini Dar es Salaam, amefariki dunia kwa kupigwa akidaiwa kuiba mayai matatu kwenye moja ya nyumba inayofuga kuku wa mayai kwenye mtaa huo.

Kijana aliyeuawa

Mama wa kijana huyo ameomba vyombo vya sheria kuingilia kati ili haki ya mtoto wake iweze kupatikana kwani waliotekeleza tukio hilo wanawaona mtaani wakitamba kuwa hawawezi kushindana na watu wenye pesa.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Machimbo, Evana Isaya amekiri tukio hilo kutokea mtaani kwake, akidai kuwa kijana huyo aliingia kwenye nyumba ya watu usiku hivyo akashambuliwa hadi kufikia umauti wake, huku akiomba wananchi kutojichukulia  sheria mkononi kwa matukio hayo.