Trump ameituhumu mahakama hiyo kwa vitendo na visivyo na msingi vinavyoilenga Marekani na mshirika wake wa karibu Israel
Hatua hiyo inaiwekea vikwazo vya kifedha na visa kwa watu binafsi na familia zao wanaosaidia katika uchunguzi wa ICC wa raia au washirika wa Marekani.
Trump alitia saini hatua hiyo wakati Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alipokuwa akizuru Washington.
Novemba mwaka jana, ICC ilitoa hati ya kukamatwa kwa Netanyahu kwa tuhuma za uhalifu wa kivita huko Gaza, jambo ambalo Israel inakanusha. ICC pia ilitoa kibali cha kukamatwa kwa kamanda wa Hamas.
Amri ya utendaji ya Trump ilisema hatua za hivi majuzi za ICC ziliweka historia ya hatari ambayo inahatarisha Wamarekani kwa kuwaweka kwenye unyanyasaji na uwezekano wa kukamatwa
Trump anasema Tabia hii inatishia kukiuka uhuru wa Marekani na inadhoofisha kazi muhimu ya usalama wa kitaifa na sera ya kigeni ya serikali ya Marekani na washirika wake ikiwa ni pamoja na Israel
Marekani si mwanachama wa ICC na mara kwa mara imekataa mamlaka yoyote ya chombo hicho juu ya maafisa wa Marekani au raia.