Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Kuu jijini Dar es Salaam imegiza shauri la Dkt. Wilbroad Slaa lirejeshwe Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwaajili ya kushughulikiwa kwa dhamana yake
Dkt. Slaa na Mawakili wake walifungua shauri la mapitio la kesi yake katika Mahakama Kuu akipinga mwenendo wa Mahakama ya Kisutu kuahirisha usikilizwaji wa dhamana yake kutokana na maombi ya kupinga dhamana yaliyotolewa na Jamhuri
Dkt. Slaa alikosa dhamana tangu alipofikishwa Mahakamani Januari 10, 2025 kusomewa shtaka linalomkabili la kusambaza taarifa za uongo kupitia Mtandao wa X.