Friday , 17th Jan , 2025

Pablo Picasso aliwahi kunukuliwa ''Good artists copy, great artists steal'' akiwa na maana wasanii wazuri ni wale wanaochukua kazi za wengine na kuzifanya kama zilivyo ila wasanii bora ni wale wanaoiba kazi hizo na kuzifanya kwenye namna ya tofauti.

Leo nizungumze na watayarishaji wa maudhui kidogo, hivi Ilishawahi kutokea siku kwenye kazi zako umekutana na picha ambayo ulitamani sana kuitumia lakini isivyo bahati picha hiyo ina copyright?

Nakupa wavuti ambayo unaweza kuitumia kubadili picha ambayo ulishindwa kuitumia kwa sababu za copyright, kuifanya kuwa picha ya tofauti na ukaweza kuitumia kwenye ubunifu wako mtandaoni.

Wavuti yenyewe inaitwa ''NoMoreCopyright.com''

Kinachofanyika kwenye wavuti hii ni kukupa upande wa kipekee na wa tofauti wa ile picha ambayo unatamani kuitumia kwenye mtandao na ikaja kwenye utofauti ambao haitaleta tena changamoto za copyright.