Wednesday , 1st Jan , 2025

Bei za vyakula na bidhaa katika siku kuu ya mwaka mpya zimeendelea kupaa huku kukua kwa mahitaji ikilinganishwa na uwepo wa bidhaa husika sokoni, kumetajwa kuwa sababu ya ongezeko la bei.

watu wanataka wakapike kwao unakuta kama hii miguu ya kuku na utumbo hawanunui

Bei za vyakula na bidhaa katika siku kuu ya mwaka mpya zimeendelea kupaa huku kukua kwa mahitaji ikilinganishwa na uwepo wa bidhaa husika sokoni, kumetajwa kuwa sababu ya ongezeko la bei.

Katika kusherehekea Siku kuu ya Mwaka mpya baadhi ya bidhaa zimepanda bei huku ikisababisha ugumu kwa wanunuzi pamoja na baadhi ya wafanyabishara kukosa faida kwa kuuza bei ileile huku wakiwa wamenunua kwa bei ya ghali.

"Kwakweli siku ya leo bei zimepanda sana mfano nyama sehemu zingine watu wananunua mpaka 14,000 kwa kilo nawakati ilikuaga 10,000 mpaka 11,000 mpaka unatamani sikukuu ziishe kwakweli". Amesema Anna Brayson Chilale, Mkazi wa Mwananyamala kwa Kopa Dar es Salaam.

"Bei kwa leo zipo juu sana halafu unakuta mtu anakuja hapa inabidi umuuzie chakula kwa bei ileilee ya 2,000 huku wewe unakuwa umenunua gharama inakua inakukosesha faida kabisa". Amesema Christina Exaveli John, Mama lishe Soko la Mapinduzi Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanya biashara sokoni hapo wameeleza kuwa kwa sikukuu ya leo baadhi ya zimepanda kwa kuwa mahitaji yanakuwa juu huku upatikanaji ukiwa mgumu.

"Kwenye hizi sikukuu hapa sokoni bei zinakuwa zinapanda ila kwasababu hii tunajua bei huwa hazigandi zinabadilika na hapa sikukuu zikiisha tutashuhudia bei zinashuka kama kawaida kwa sababu ya mahitaji".  Amesema Hassan Nguya Madika, Mwenyekiti wa soko la Mapinduzi Dar es Salaam.

"Leo hapa sokoni kama hivi kuku unakuta watu wengi wanakula kawaida na leo watu wanataka wakapike kwao unakuta kama hii miguu ya kuku na utumbo hawanunui sasa unakosa hela ya kuwalipa wachinjaji inamana inabidi tuuze vyote kwa pamoja ili kupata hela yakufidia". Amesema Juma Msagati, Mfanyabiashara wa Nyama ya Kuku Mapinduzi Dar es Salaam.

"Kwa sisi hivi mchele unakuta upo tuu lakini kule tunaponunua unakuta watu wengi na wauzaji hamna na wameenda kwenye sikukuu huku nasisi tunakosa namna yakufanya inabidi tuuze huohuoo uliopo hapa". Amesema Abdulrazak Abas, Mfanyabiashara ya Mchele Soko la Mapinduzi Dar es Salaam.

Hali hii ya kupaa kwa bei za vyakula na bidhaa ikiwaathiri wananchi wa hali ya chini na wafanya biashara wengine wakitumia kama fursa ya kutengeneza faida zaidi.