Utaratibu wa kutoa zawadi zinazoweza kuacha alama kwa wanawazawadia ili waendelee kuwakumbuka kwa ukarimu waliouonesha kwao.
Wananchi wamwkumbusha kuwa na utaratibu wa kutoa zawadi zinazoweza kuacha alama kwa wanawazawadia ili waendelee kuwakumbuka kwa ukarimu waliouonesha kwao.
Wito huo umetolewa na Abdilah Mlapakolo, Mtaalam wa malezi, mahusiano na saikolojia wakati wa mahojiano yake katika kipindi cha SuperBreakfast asubuhi ya leo huku akielezea umuhimu wa kutoa zawadi.
“Zawadi inaweza kuwa kitu chochote lakini zawadi ya kitu ni nzuri kwa sababu mtu ataendelea kukitumia tofauti na zawadi ya chakula kwani inawahi kusahaulika”, Abdilah Mlapakolo - Mtaalam wa malezi, mahusiano na saikolojia.
EATV ikatembelea baadhi ya mitaa nao wanaelezea uelewa wao na namna gani huwa wanashiriki kutoa zawadi kwa wapendwa wao.
“Binafsi sielewi chochote kuhusu utoaji wa zawadi labda kwa sababu nimetokea kijijini huko hatukuwa na kawaida ya kutoa zawadi”, NASSOR SALUM-Mkazi wa Dar es Salaam.
“Mimi musilam utaratibu wangu huwa natoa zaka pamoja na zawadi kwa watu wenye uhitaji na wasiojiweza”, ABUU ISSA-Mkazi wa Dar es Salaam
“Mimi sina wakati maalum wa kutoa zawadi, nikijua kitu fulani nikimpa mtu fulani atafurahia basi huwa nafanya hivyo sisubiri wakati wa sikukuu”, HAROUN SADDY-Mkazi wa Dar es Salaam.