Saturday , 7th Dec , 2024

Muigizaji Monalisa ameendelea kupigia mistari msemo wa 'Usimkatie mtu tamaa' baada ya kuwajibu waliomsema amezeeka na kumcheka kurudi kusoma kwa kigezo cha umri.

Picha muigizaji Monalisa

Monalisa ameshea hilo baada ya kuhitimu Biashara na Usimamizi wa Miradi na kuwa muhitimu bora aliyefanya vizuri.

"Walisema nimeshazeeka kwanini nirudi shule? Kufanya nini? Na wengine walinicheka sana kuniona naingia darasani na hawakuamini kwenye dhana ya kuanza upya"

"But today, I proudly graduate in Business and Project Management as the eldest in my class na NIMEBUTUA hasa (BEST PERFORMING GRADUANT). Huu ni ushuhuda wa uvumillivu, ujasiri na uthubutu" ameandika Monalisa

Una mpango wowote wa kurudi darasani kusoma tena?