Monday , 2nd Dec , 2024

Kama ulikuwa unahitaji kufanya mazoezi iwe ni kupunguza mwili au kukaza misuli kwa lengo la kuongeza ukakamavu wa mwili, lakini ulikosa msaada na njia ambayo utaweza kutumia kwenye hilo.

 

Mimi leo nakupa msaada kwenye hilo kwa kukutaji wavuti ambayo inaweza kukusaidia kwenye hilo, wavuti yenyewe inaitwa Musclewiki.com kupitia wavuti hii utafanikiwa kupunguza mwili na kujenga misuli kwa kuchagua eneo husika ambalo wewe unahitaji kulifanyia kazi mfano unahitaji kupunguza tumbo, ukishaingia kwenye wavuti hii utagusa eneo la tumbo kwenye mchoro ambao utajitokeza na baada ya hapo zitatokea video mbali mbali ambazo zinaonesha mazoezi ya kuzingatia ili ufanikiwe kupunguza tumbo

 

Na kutokea hapo sasa kilichobaki ni utekelezaji kama miradi ya serikali, karibu sana, na hii ndiyo SupaTech