Friday , 22nd Nov , 2024

Jeshi la Polisi nchini limetakiwa kuongeza nguvu kwenye rasilimali watu, vifaa na uwekezaji kwenye tehama ili kupambana na uhalifu wa mitandaoni ambao umekuwa ukisababisha changamoto kwa wananchi.

Waziri wa mambo ya ndani, Mhandisi Hamad Masaunui

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni, mara baada ya kumaliza kikao cha mashauriano ni namna gani uhalifu wa mitandaoni unaweza kumalizwa nchini.
"Jeshi la Polisi liongeze nguvu kwenye rasilimali watu, fedha, vifaa pamoja na tehama lakini pia maazimio yetu mengine tumeunda task force , itakayoanza kazi mara mohja kwa ajili ya kufanya ufatiliaji wa utapeli mitandaoni, matangazo ya udhalilishaji pamoja na wezi wa mitandaoni", Mhandisi Hamad Masauni-Waziri wa mambo ya ndani ya nchi.

Aidha wananchi wametakiwa kuhakiki namba zao za NIDA ili kujua namba ngapi zimesajiliwa kwa namba hiyo.
"Niwaombe wananchi kuhakiki namba zao za NIDA, ili kujua zimesajili namba ngapi ambazo ziko hewani ili kupunguzwa kwenye usajiloi wake, hii inaenda sambamba na makampuni ya simu kumarisha sajili za namba za simu", Jerry Silaa-Waziri wa Habari.

Nao baadhi ya wananchi wameomba Serikali kuongeza ufatiliaji ili kupunguza uhalifu wa mitandaoni.
"Mimi binafsi sina mamlaka ya kujua anaefanya utapeli ni nani lakini hizi namba hazifanyi kazi bila usajili kwahiyo Serikali ikifanya ufatiliaji kuanzia namba hiyo inasoma jina gani na inapatikana maeneo gani ni rahisi kugundua ni nani anahusika na uhaifu huo", Ambokile Mwamafupa-Mkazi wa Dar es Salaam.

"Kila kitu kina miziz yake, nafikiri mizizi ingeangaliwa imeanzaje, ili kuweza kudhibiti matawi yake, yasiendelee lusambaa , kwahiyo nashauri mamlaka husika ziongeze nguvu za kuwakamata na adhabu wanazokutana nazo hiyo itasaidia wengine kuendelea na utapeli huo", Mwinyi Ally-Mkazi wa Dar es Salaam.