Tuesday , 19th Nov , 2024

Wachimbaji Nchini wameiomba Serikali kuwawezesha Mashine za uchorongaji miamba, ili kuongeza uzalishaji na uaminifu kwenye taasisi za kifedha ili waweze kukopesheka na kuongeza mitaji yao.

Victor Tesha, Makamu wa Rais wa shirikisho la wachimbaji Tanzania (FEMATA).

Ombi hilo limetolewa na Makamu wa Rais wa shirikisho la Wachimbaji Madini nchini, Victor Tesha kwenye ufunguzi wa Mkutano wa kimataifa wa uwekezaji kwenye  sekta ya Madini uliofanyika Leo jijini Dar es Salaam.
“Ombi letu kubwa Mashine ya kuchorongea miamba walau zifike kila wilaya zitasaidia kupata data za kutosha ili tuweze kukopesheka kwenye mabenki kulingana na rasilimali zilizopo”, Victor Tesha, Makamu wa Rais FEMATA.

Mkutano wa Kimataifa wa uwekezaji kwenye sekta ya Madini umelenga kuongeza thamani kwa madini yaliyopo nchini, Makamu wa Rais wa Mgodi wa Geita, Simon Shayo, anasema wameanza mazungumzo na Benki Kuu ili waanze kuwauzia dhababu iliyoongezewa thamani nchini.
“Mgodi wa Geita umekuwa ukichakata Dhahabu hapahapa nchini, na tumeanza mazungumzo na Benki kuu ili tuanze kuwauzia dhahabu iliyochakatwa”, Simon Shayo, Makamu wa Rąis GGML.

Kuhusu uongezwaji wa thamani Madini nchini, waziri wa Madini Antony Mavunde anasema sheria ipo tayari huku akielezea faida zake.
“Tutaongeza ajira kwa watanzania, mapato lakini pia hatutatoa tena leseni kubwa kwa wawekezaji wakubwa mpaka waweke sera ya kufanya uchakataji wa uongezaji wa thamani hapahapa nchini kwetu”, Antony Mavunde, Waziri wa Madini.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameziagiza wizara za kisekta kuhakikisha zinaondoa changamoto ili kuvutia uwekezaji kwenye sekta hiyo.
“Wizara endeleeni kusimamia vyama viweze kufuata sheria, sera na taratibu, Aidha wachimbaji wote wanatakiwa wauze 20% kwa benki kuu, Tanesco hakikisheni huduma inafika kwenye migodi yote nchini na wawekezaji karibuni kuwekeza Tanzania kwani kuna mazingira bora ya uwekezaji”, Kassim MajaliaASSIM MAJALIWA-Waziri Mkuu.