Wednesday , 6th Nov , 2024

Michezo ya ligi kuu Tanzania bara itaendelea leo na kesho kwa michezo kuchezwa viwanja tofauti nchini, leo Novemba 6 uwanja wa KMC Complex utachezwa mchezo utakaozikutanisha timu za Simba SC dhidi ya KMC FC na Kesho Yanga SC itakipiga dhidi ya Tabora United  Azam Complex Chamazi Dar es sal

Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kinashika nafasi ya tatu msimamo wa ligi kuu TPL kikiwa na alama 22 nyuma ya Singida Black Stars yenye alama 23 Yanga SC ikiwa kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 24.

Michezo ya ligi kuu Tanzania bara itaendelea leo na kesho kwa michezo kuchezwa viwanja tofauti nchini, leo Novemba 6 uwanja wa KMC Complex utachezwa mchezo utakaozikutanisha timu za Simba SC dhidi ya KMC FC na Kesho Yanga SC itakipiga dhidi ya Tabora United  Azam Complex Chamazi Dar es salaam. 

Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kinashika nafasi ya tatu msimamo wa ligi kuu TPL kikiwa na alama 22 nyuma ya Singida Black Stars yenye alama 23 Yanga SC ikiwa kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 24.

Michezo ya leo na kesho itatoa picha ya timu itakayokaa kileleni mwa ligi mpaka pale itakaporejea baada ya kupisha ratiba timu za taifa zitazochezwa wiki ijayo. Yanga SC ilipoteza dhidi ya Azam mwishoni mwa Juma lililopita kufanya mbio za ubingwa kubaki wazi kutokana na utofauti wa alama zinazotenganisha timu hizo.

Kikosi kinachonolewa na Fadlu Davids raia wa Afrika ya Kusini kama kitaondoka na ushindi dhidi ya KMC kitafikisha alama 25 kitapanda mpaka nafasi ya kwanza kwa muda kabla ya Watani wao wa Jadi Yanga SC  kucheza kesho Novemba 7 dhidi ya Tabora United.

Ubingwa wa ligi kuu msimu huu unatizamiwa utakuwa mgumu kutokana na uwekezaji uliofanywa kwenye timu nyingi zinazoshiriki ligi.Mabingwa wa zamani wa Tanzania Simba imesajili Wachezaji wengi walioongeza ubora na ushindani wa ligi Washambuliaji Leonel Ateba,Valentino Mashaka na Steven Mukwala wote wamefunga goli mbili kila mmoja mpaka sasa safu ya kiungo Yusuph Kagoma, Debora Fernandes, Augustine Okejepha na Awesu Awesu wameongeza uimara eneo hilo muhimu la timu iwapo uwanjani.

Singida Black Stars nayo haiko nyuma inafukuza mwizi kimyakimya hakuna ambaye alikuwa anafahamu kabla ligi kuanza kama timu hiyo ingeshika nafasi iliyopo baada ya michezo 10 ya ligi kuu, uwepo wa Kocha Patrick Aussems kumeongeza ubora kutokana na uzoefu wake wa ligi kuu na mpira wa Afrika kwa ujumla,ufahamu wa jinsi ya kuishi na Wachezaji wa Kiafrika kumeifanya Singida Black Stars kushangaza Wadau wengi wa soka Tanzania kutokana na ushindani inaouonyesha msimu huu wa 20224-2025.

Yanga SC itakipiga kesho na Tabora United ikipania kufuta maumivu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Azam na ushindi wa kesho utakiwezesha kikosi cha Kocha raia wa Argentina Miguel Gamondi kuendeleza kung'ang'ania kileleni mwa ligi kwa taofauti wa alama tatu dhidi ya Singida Black Stars na alama mbili mbele ya Wekundu wa Msimbazi kama nayo itashinda dhidi ya KMC FC leo.