Monday , 20th Jun , 2016

Vilabu shiriki vya ligi nchini vimetakiwa kuchagua magoli kipa kutoka ndani ya nchi ambao watahakikisha watakuwa nao na kuweza kuwakuza kwa ajili ya timu za taifa.

Kocha wa kituo cha kukuza vipaji vya magolikipa nchini Peter Manyika amesema, vilabu vinatakiwa kuamini vyakwao kwani kipa anayotoka katika vitu vya kukuza vipaji anauwezo wa kufanya majaribio sehemu yoyote na kuweza kufanya vizuri kwa manufaa ya vilabu vya ndani.

Manyika amesema, vilabu vinatakia kuwa na utamaduni wa kuangalia kwanza ndani kwani magolikipa wazuri ambao wanakosa nafasi ndani ya nchi na wengi wao hukimbilia nje suala ambalo linapelekea vilabu vingi kutafuta walinda milango nje ya nchi.

Manyiam amesema, iwapo vilabu vitakuwa makini katika kuchagua walinda milango wa ndani, kutakuwa na mabadiliko makubwa sana kwa upande wa walinda milango hapa nchini.