Tuesday , 5th Nov , 2024

Kocha wa timu ya taifa ya Burkina Faso Brama Traoré ametaja majina ya Wachezaji atakawatumia kwenye michezo miwili ya kufuzu AFCON 2025, dhidi ya timu za taifa za Senegal na Malawi jina la Mchezaji wa Yanga ya Tanzania Stephane Aziz Ki likikosekana kwenye kikosi hiko.

Kikosi cha Yanga SC kina Wachezaji wengi wanaoweza kuziba pengo la Aziz Ki kipindi atakachokosekana uwanjani ili atafute utimamu wa mwili wake Clatous Chama na Pacôme Zouzoua ni mbadala sahihi kwenye eneo la namba 10 kikosi cha Wanachi.

Maswali yamekuwa mengi kwa Wadau wa soka nchini kuhusiana na kiwango cha Mchezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania bara msimu uliopita aliyefunga goli 21. Kiungo huyo wa ushambuliaji wa kikosi cha Wana Jangwani anaonekana kuchoka msimu huu kutokana na aina ya uchezaji wake kwa ujumla kuanzia kwenye kufanya maamuzi awapo uwanjani kwani anapoteza sana mpira tangu msimu huu uanze.

Aziz Ki alikuwa silaha muhimu kwa Gamondi msimu uliopita alionekana kuwa fiti kwenye kila kitu uwanjani mikimbio, kuchezesha wengine, kupiga pasi za kuzalisha magoli pamoja na kufunga yeye mwenyewe msimu 2024-2025 umekuwa mgumu kwakena takwimu zinaonyesha hivyo.

Sababu mbalimbali zinatajwa kuhusishwa na kushuka kiwango kwa Kiungo huyo wa zamani wa Rayo Vallecano, ASEC Mimosas anagawanya mawazo ya Mashabiki wa Yanga kuna baadhi wanaamini anapswa kupumzika ili arudi akiwa sawa kwenye michezo ya ligi kuu pamoja na klabu bingwa ya Afrika wengine wakiamini anapaswa kuendelea kucheza atarejesha kiwango chake kwa kucheza michezo mfululizo.

Msimu uliomalizika wa ligi kuu Tanzania bara MVP wa TPL alihusika na upatikanaji wa magoli 29 akisaidia goli 8 na kufunga 21. Kazi inabaki kwa Miguel Gamondi kuamua kuendelea kumtumia raia huyo wa Burkinabe au ampumzishe arudi kwenye ubora wake amsaidie katika mikikimikiki ya klabu bingwa barani Afrika.

Kikosi cha Yanga SC kina Wachezaji wengi wanaoweza kuziba pengo la Aziz Ki kipindi atakachokosekana uwanjani ili atafute utimamu wa mwili wake Clatous Chama na Pacôme Zouzoua ni mbadala sahihi kwenye eneo la namba 10 kikosi cha Wanachi.

Kukosekana kwa Stephane Aziz Ki timu yake ya taifa ni ishara tosha kwa Kocha raia wa Argentina katika klabu wenye makao makuu yake mitaa ya Twiga na Jangwani kwamba anapaswa kumtizama mchezaji wake kwa jicho la tatu kwani kiwango chake hakiposawa na baadhi ya Mashabiki wakisema kuyumba kwa kiwango cha kikosi hiko imesababishwa na Azizi Ki kutokuwa sawa kiuchezaji.