Monday , 4th Nov , 2024

Kocha mwenye maneno mengi barani Ulaya anayefundisha klabu ya Fenerbahçe SK amembwatukia Refarii aliyechezesha mchezo kati ya Sivasspor dhidi ya kikosi cha Mourinho ambao ulimalizika kwa kikosi cha Fenerbahçe SK kuondoka na ushindi wa goli 2-3.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea FC, Manchester United na Tottenham Hotspurs anasifika kwa uwezo wa kushinda ubingwa na timu zake zote alizowahi kuzifundisha anatumainiwa na Mashabiki wa Fenerbahçe SK kurudisha furaha yao kwa kushinda ubingwa wa Super Lig  muda mrefu kwa klabu hiyo umepita bila kushinda ubingwa wa nchi hiyo.

Kocha huyo raia wa Ureno amesema timu yake inaonewa kwani kwenye mchezo wa jana Wapinzani wake hawakustahili kupata penati mbili pia alitanabaisha timu yake ilipaswa kupata penati kabla ya kupata goli la ushindi lililofungwa na Sofyan Amrabat dakika ya 102.

Mourinho alienda mbali kwa kumbwamia Muamuzi huyo kama angefahamu upungufu wao mapema asingekubali kabisa kufundisha mpira nchini Uturuki. The Special One anafahamika kwa kutoa maneno ya hovyo kwa Marefarii na Makocha wa timu pinzani ambapo mara kadhaa imemsababishia kujikuta matatizoni na Mamlaka ya soka nchi mbalimbali alizowahi kufundisha Mreno huyo.

Kabla ya kujiunga na Mabingwa hao wa mwaka 2013 wa ligi kuu ya Uturuki alihudumu kikosi cha AS Roma cha nchini Italia ambacho alikiongoza kushinda ubingwa wa UEFA Conference League na kucheza fainali ya UEFA Europa League dhidi ya Sevilla lutoka nchini Hispania ambayo Roma ilipoteza.

Kikosi cha Fenerbahçe SK kinashika nafasi ya pili msimamo wa ligi ya Uturuki Süper Lig itakuwa na mtihani mkubwa siku ya Alhamis Novemba 7 ugenini nchini Uholanzi dhidi ya AZ Alkmaar mchezo wa kombe la Shirikisho barani Ulaya.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea FC, Manchester United na Tottenham Hotspurs anasifika kwa uwezo wa kushinda ubingwa na timu zake zote alizowahi kuzifundisha anatumainiwa na Mashabiki wa Fenerbahçe SK kurudisha furaha yao kwa kushinda ubingwa wa Super Lig  muda mrefu kwa klabu hiyo umepita bila kushinda ubingwa wa nchi hiyo.

Mourinho amewahi kujikuta matatizoni na Mamlaka ya soka kwenye nchi zote alizofundisha soka kutokana na kuzisemea mambo mamlaka hizo Makocha wa timu Pinzani na Marefarii inakumbukwa alishawahi kukunjana mashati na Kocha wa zamani wa Arsenal ya Uingereza Arsène Wenger baada ya kumita Mkufunzi huyo mwenye heshima kubwa kwenye klabu ya Washika mitutu wa London bingwa wa kufeli iliyopelekea Wenger kupata hasira na kuchukizwa na maneno ya Mourinho.