Thursday , 31st Oct , 2024

Kocha wa muda klabu ya  Manchester United Ruud Van Nistelrooy ameanza kwa ushindi kwenye kibarua chake cha kuifundisha timu ya Mashetani Wekundu  kwa kuiongoza kushinda mchezo dhidi ya Leicester City goli 5-2 kwenye uwanja wao wa  nyumbani Old Trafford.

Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu ya Uingereza waliikaribisha Leicester City kwenye mchezo wa mzunguko wa 4 wa kombe la ligi Carabao na kupata ushindi mnono wa goli 5-2. hiyo ni idadi kubwa ya goli ambazo United imefunga msimu huu kwenye mchezo mmoja. 

Man U ilimfukuza kazi kocha wake Erik Ten Hag siku ya Jumatatu na Mholanzi mwenzake Mshambuliaji wa zamani wa Masheatani Wekundu kupewa nafasi ya kukiongoza kikosi hiko  kwa muda mpaka pale klabu itakapomtangaza Mwalimu mkuu mpya. Van Nistelrooy amewahi kuiongoza klabu ya PSV Eindhoven kabla ya kujiunga na United kusaidiana na Ten Hag mwanzoni mwa msimu wa 2024-2025.

Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu ya Uingereza waliikaribisha Leicester City kwenye mchezo wa mzunguko wa 4 wa kombe la ligi Carabao na kupata ushindi mnono wa goli 5-2. hiyo ni idadi kubwa ya goli ambazo United imefunga msimu huu kwenye mchezo mmoja. 

Bruno Fernandes, Casemiro walifunga goli 2 kila mmoja, Alejandro Garnacho alifunga moja  shangwe za  Mashabiki wa United zilisikika kwa sauti kubwa baada ya kukatishwa tamaa walionyesha kukata  kulikosababishwa na matokeo mabovu kwenye timu hiyo kwa muda mrefu. Wachezaji walijituma walipambania kila mpira ambao walipaswa kuupambani pale walipopoteza mpira na kulikua na mipango ya kutafuta magoli kitu ambacho hakikuwepo huko nyuma chini ya kocha wao wa zamani.

Mabosi klabu hiyo yenye makao yake kwenye Jiji la Manchester wapo kwenye mpango wa kumsajili Kocha kutoka Sporting Lisbon ya Ureno Ruben Amorim kuliongoza jahazi hilo liloonekana kumshinda Nahodha wao wa zamani waliyemtimua kazi.

Manchester United itakabiliana na Chelsea FC kwenye mwendelezo wa michezo ya ligi kuu Uingereza EPL siku ya Jumapili uwanja wa Old Trafford, kwa mujibu wa vyombo vya habari vinavyoripoti habri za michezo Ulaya zimebainisha timu hiyo inaweza kumtangaza Ruben Amorim kuwa Kocha wao mkuu siku ya leo Oktoba 31 2024.