Wednesday , 30th Oct , 2024

Taifa Stars imeshafuzu michuano hiyo kupitia tiketi ya Uenyeji wa mashindano hivyo inahitaji ushindi katika mchezo huo ili kurejesha imani kwa Watanzania kwenye timu ya taifa baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya Congo DRC,  kufuzu michuano ya AFCON 2025 nchini Morocco.

Mchezo wa marudiano wa kufuzu kushiriki michuano ya CHAN 2025 kati ya timu ya taifa Taifa Stars dhidi ya Sudan uliopangwa kuchezwa uwanja wa Benjamini Mkapa hautokuwa na kiingilio ili kuwezesha Watanzania wengi kuingia uwanjani kuishanglia timu ya taifa baada ya kupoteza mchezo wa kwanza ugegeni nchini Mauritania kwa kufungwa goli 1-0.

Mchezo wa marudiano wa kufuzu kushiriki michuano ya CHAN 2025 kati ya timu ya taifa Taifa Stars dhidi ya Sudan uliopangwa kuchezwa uwanja wa Benjamini Mkapa hautokuwa na kiingilio ili kuwezesha Watanzania wengi kuingia uwanjani kuishanglia timu ya taifa baada ya kupoteza mchezo wa kwanza ugegeni nchini Mauritania kwa kufungwa goli 1-0.

Shirikisho la mpira Tanzania TFF limetoa tamko hilo kuelekea mchezo huo utakaochezwa Novemba 3, 2024. Kumekuwa na kasumba ya Watanzania kutokwenda kuishangilia timu yao inapocheza na TFF imeona isiweke kiinglio mchezo huo ili kuwavutia Mashabiki wengi kwenda uwanja wa Benjamini Mkapa kuitizama na kuisapoti Stars.

Taifa Stars imeshafuzu michuano hiyo kupitia tiketi ya Uenyeji wa mashindano hivyo inahitaji ushindi katika mchezo huo ili kurejesha imani kwa Watanzania kwenye timu ya taifa baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya Congo DRC,  kufuzu michuano ya AFCON 2025 itakayofanyika nchini Morocco.

Mwalimu anayekiongoza kikosi cha Stars kwenye michezo dhidi ya Sudan ameita Wachezaji wengi wasio na uzoefu na timu ya faifa ili waweze kupata uzoefu wa michezo mikubwa na wawe tayari kuitumikia timu ya taifa pale watakapohitajika na pasiwe na kigezo cha kukosa uzoefu wa michezo ya kimataifa.

Mchezo wa Novemba 3 ni muhimu kwa timu yetu ya taifa, utaweza kurudisha ari ya upambanaji kuelekea michezo ya kufuzu AFCON 2025 dhidi ya Guinea na Ethiopia mchezo wa kundi H ambalo Stars inashika nafasi ya 3 nyuma ya Congo DRC inayoongoza kundi ikiwa imekusanya alama 12 baada ya kushinda nichezo minne ikifuatiwa na Guinea yenye alama 6 baada ya kucheza michezo minne.

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limetoa uwito kwa Watanzania kujenga tabia ya kuhudhuria kwenye michezo ya timu ya taifa ili kuwatia moyo Wachezaji kulipambania taifa kwa kufahamu Watanzania wapo nyuma yao tusipokwenda viwanjani tunawavunja moyo Wachezaji kwa kuhisi Watanzania hawapo nyuma yao na hawaaminiwi hivyo kuvinjika moyo.