Tuesday , 29th Oct , 2024

Rapper Wakazi ameendelea kupishana kauli na msanii mwenzie Zuchu yote haya yametokana na mjadala ambao umekuwa ukizingumziwa sana kwa siku ya jana kuhusu baadhi ya wadau na mashabiki kumshindanisha #Jide na #Zuchu katika upande wa uandishi pamoja na live performance

Pichani Ni Wakazi na Zuchu

Rapper Wakazi alitolea mtazamo wake kuhusu jambo hilo ambalo kwa namna fulani Zuchu hakupendezwa na mtazamo wa rapper huyo na kushusha ujumbe mrefu kumchana Wakazi na kusema kuwa hajui nyimbo zake.

Sasa leo kumekucha tena Wakazi amemjibu msanii huyo kupitia mtandao wa X zamani Twitter na kuandika......."Zuchu anasema hajui nyimbo zangu, ila cha ajabu alinipigia simu akaomba nimsindikize Zanzibar ana jambo lake… And she paid me for everything flight, hotel, etc (I got receipts as always) Ila pia ni sawa, maana nyimbo zangu wanaozijua wote PISI KALI!  Chief Petty Officer!'' Ameandka Zuchu

Ikimbukwe kuwa Siku ya jumamosi msanii Lady JayDee alifanya show kwenye jukwaa la Heshima ya bongo fleva linalosimamiwa na Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu (Mr Two) na huko ndiko kulikotokea maneno yote hayo baada ya Jide kufanya show nzuri na wadau kuanza kuwalinganisha wasanii hao kwenye upande huo wa kutoa burudani.