Monday , 28th Oct , 2024

Wachimbaji wadogo wa madini katika eneo la Nyarugusi mkoani Geita wamelalamikia kunyang’anywa maeneo ya uchimbaji ambayo wamekuwa wakiyavumbua na kimilikishwa kwa watu wenye vipato vikubwa (matajiri) na wao kubaki bila sehemu za kufanyia kazi

Wachimbaji hao wadogo katika wametoa kero zao katika eneo jipya la uchimbaji (rashi) lililo gunduliwa la Nyarugusi walilo vumbua hivu karibuni ambapo wamesema moja ya kero kubwa wanayokumbana nayo ni ya kunyanganywa migodi pindi tu wanapoianzisha na migodi hiyo kuanza kuonesha kupatikana kwa dhahabu wanaletwa watu wenye vipato na kumilikishwa migodi hiyo.

“Sisi wachimbaji vijana kuna changamoto nyingi sana tunazozipitia kama kuvumbua maeneo lakini wanakuja kukabidhiwa watu wengine rashi na sisi tunashindwa kukabidhiwa hizo rashi pendine ni kwa sababu ya elimu au matajiri wanaokuwa na fedha wanaoweza kupokonya nafasi hizi na hata hatujawahi kupewa hata elimu ya uchimbaji.” Amesema Mohamed Yusuph mchimbaji mdogo.

Aidha viongozi wa wachimbaji vijana mkoa wa geita wamefika eneo hilo jipya kusikiliza baadhi ya changamoto hizo zinazo wakumba vina hao na kuahidi kuzishughulikia ikiwemo kuhataka kuunda vikundi vitakavyo wawezesha kupata elimu ya uchimbaji pamoja na kupata leseni zitakazo weza kuwatambua kama wachimbaji wadogo.