Thursday , 24th Oct , 2024

Serikali inakuja na mpango wa kuongeza misitu ya asili kwa kila halmashauri nchini kuwa na msitu wake ikiwa moja ya njia ya Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira ambapo baadae itasaidia kwenye biashara ya kaboni

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Ashatu Kijaji ameyasema hayo mkoani Tanga wa ziara yake ya kikazi ya kukagua, kufugua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo.

Kijaji ameeleza kuwa lengo ni halmashauri hizo kuingia kwenye biashara ya Kaboni ambapo zoezi la kupandwa miti kwa pamoja kutawezesha faida kuonekana haraka kuliko kupandwa na mtu mmoja mmoja.

Waziri Kijaji ameongeza, mpango huo utashirikisha hasa wale ambao wana maeneo makubwa ya ardhi ambapo wanaweza kutumia ekari tano mpaka kumi kwa ajili ya kupanda miti hiyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Burian amesema kumekuwepo changamoto ya wananchi kuchoma misitu hovyo na hivyo wamekuwa wakiendelea kutoa elimu kwa wananchi kuona jinsi ya kuzuia matukio hayo.