Wajumbe hao wamalalamikia wizi wa kura uliofanywa na baadhi ya viongozi ikiwa diwani wa kata hiyo ambapo wameeleza baadhi ya wanachama kufukuzwa na kutokupiga kura na baadae matokeo kuzidi idadi ya wapiga kura.
“Kura za Wajumbe tumepata 297, ila kura za wenyeviti tumehesabu zimefika 548 kwa hiyo tumetoka hapa mpaka wilayani kushtaki wametuambia wanakuja wasipokuja kutatua hili tunaenda mkoani. Tumeshalalamika sana Mwenyekiti wa kata na Diwani wanatuhujumu na wakina mama wamefukuzwa kupiga kura na tunachokizungumza hapa hatumtaki diwani” Amesema Moja ya Mjumbe wa CCm Kata ya mwanga Kigoma.
Wananchi na wanachama wa chama cha Mapinduzi kata hiyo wamesema hawana Imani na diwani wa kata ya mwanga katika uchaguzi huo wa kura za maoni kwani amekuwa akiendeleza vitendo visivyofaa na kuvuruga mchakato wa uchaguzi jimboni.
Sambamba na hilo wananchi wameonesha kutokuwa na Imani na kituo cha kupiga kura na jinsi uendeshwaji mzima wa mchakato wa uchaguzi katika kituo cha mwanga mkoani kigoma.