Klabu ya Coastal Union ya Tanga imemtangaza Juma Mwambusi kuwa kocha mkuu wa timu hiyo baada ya kumfuta kazi aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo David Ouma raia wa Kenya mwezi Agosti 2024. Kikosi hiko cha Wagosi wa Kaya kilikuwa chini ya Joseph Lazarao ambaye alikaimu kwa muda kipindi ambacho timu hiyo ilipokuwa inatafuta Mwalimu Mkuu.
Klabu ya Coastal Union ya Tanga imemtangaza Juma Mwambusi kuwa kocha mkuu wa timu hiyo baada ya kumfuta kazi aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo David Ouma raia wa Kenya mwezi Agosti 2024. Kikosi hiko cha Wagosi wa Kaya kilikuwa chini ya Joseph Lazarao ambaye alikaimu kwa muda kipindi ambacho timu hiyo ilipokuwa inatafuta Mwalimu mpya.
Mwambusi anauzoefu mkubwa wa kufundisha ligi Kuu ya Tanzania baada ya kuhudumu kwenye nafasi ya Kocha mkuu na Msaidizi kwenye timu mbalimbali nchini.
Coastal Union imekuwa na utaratibu wa kutokukaa na Makocha kwa muda mrefu kwa siku za karibuni kikosi hiko kiliachana na Ouma kabla ya msimu wa ligi wa 2024-2025 kuanza kutokana na matokeo yaliyoyapata klabu hiyo Mabingwa wa Tanzania mwaka 1988 kwenye mashindano ya kombe la shirikisho barani Afrika. Msimu wa nyuma yake iliachana na Mkufunzi mwenye mbwembwe nyingi raia wa Congo DRC Mwinyi Zahera.
Wana Mangushi ilimaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa TPL msimu uliopita wa 2023-2024 na kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya shirikisho Afrika na kutolewa hatua za awali na timu ya Bravos FC kutoka Angola. Kikosi hiko kilichohamishia kambi yake kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha inashika nafasi ya 9 kwenye msimamo wa ligi ya Tanzania ikijikusanyia alama 8 msimu huu wa 2024-2025.
Kocha Mwambusi amewahi kuzifundisha klabu kadhaa ikiwemo Mbeya City, Yanga, Azam pamoja na Ihefu. Kibarua chake cha kwanza kitakuwa Oktoba 26 Coastal Union itakapoikaribisha timu ya Yanga Sc mchezo utakaochezwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.