Naibu waziri wa kilimo David silinde amewataka viongozi wa vyama vya ushirika kutumia mifumo ya kisasa ya tehama na kuacha kutumia mifumo ya zamani ili waweze kutoa huduma bora katika vyama .
Silinde ametoa wito huo leo October 21 katika Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya ushirika wa akiba na mikopo ya mwaka 2024 yanayofanyika jijini mwanza katika uwanja wa mirongo ambapo amesema matumizi ya tehama niyalazima kama wanataka kuwahudumia wanachama vyema na kuhimili ushindani uliopo kwenye soko la fedha waache kujiebdesha kimazowea.
Nae mwenyekiti wa bodi ya chama kikuu cha ushirika wa akiba na mikopo Tanzania SCCULT . Mwl . Aziza Mshana na Benson Diego wamesema wamekuwa wakifanya maadhimisho hayo kwa kila mwaka kwa malengo kuwakumbuka na kuwaenzi waasisi wa ushirika wa akiba na mikopo kwa mchango wao mkubwa wa kueleza dhana ya akiba na mikopo duniani na Tanzania kwa ujumla .
Maadhimisho haya hayo yanafanyika kwa Siku 5 kuanzia October 20 mwaka huu hadi October 24 mwaka huu yenye kauli mbiu inayosema " ulimwengu mmoja kupitia ushirika wa kifedha " ambayo yana adhimishwa kwa mara ya 76 duniani na kwa mara ya 15 kwa nchini Tanzania tangu kuanzishwa kwake .