Wachezaji wa timu za taifa za Wanawake zaidi ya 100 wameliandikia barua ya wazi Shirikisho la mpira Duniani FIFA kulitaka kuvunja mkataba wake wa udhamini na kampuni ya mafuta ya Saudi Arabia ya Aramco. Sababu kubwa zilizotajwa na Wachezaji hao ni kutokana na uharibifu wa Mazingira unaofanywa na kampuni hiyo ya uchimbaji wa mafuta, pamoja na uvunjwaji wa Haki za Binadamu nchini SaudI Arabia. Uwepo wa tamaduni ambazo zinamkandamiza Mwanamke nchini humo inatizamwa kama sababu kubwa zaidi ya Wachezaji wa timu za Wanawake kugomea mkataba huo wa udhamini. Aramco imesaini mkataba na FIFA utakaofika tamati mwaka 2027 ambapo kampuni hiyo itadhamini kombe la Dunia la Wanaume 2026 na Wanawake 2027.
Wachezaji zaidi ya 100 wameugomea udhamini wa kampuni ya uchimbaji wa Mafuta ya Aramco yenye makoa makuu yake nchini Saudi Arabia. Wachezaji hao wameweka wazi kutokuridhishwa na mkataba ambao FIFA umesaini na kampuni hiyo kutokan na kukiuka kauli mbiu na miongozo ya Shirikisho la mpira Duniani.
Aramco kampuni inayojihusisha na uchimbaji wa mafuta kutoka Saudi Arabia imesaini mkataba utakaotamatika mwaka 2027 baada ya fainali za kombe la Dunia la Wanawake. Saudi Arabia inatuhimiwa kwa uvunjwaji wa Haki za Binadamu sambamba na uwepo wa Tamaduni ambazo zinamnyima haki Mwanamke kujihusisha na maswala ya kimichezo ikiwemo kutokuhudhuria viwanjani.
Vivianne Miedema Mshambuliaji wa timu ya Wanawake Manchester City ambaye pia ni mmoja wa waliotia saini pingamizi hilo kwa FIFA amesema wao kama Wachezaji wanatakiwa kuonyesha wanajali pamoja na kuhakikisha kizazi kijacho kinakuta mazingira rafiki ya kuishi.
Sofie Junge Pedersen amesema wanalitaka shirikisho hilo kubadili Mdamini kwa kutafuta kampuni ambayo inajali Haki za Binadamu, Usawa wa Kijinsia na Dunia iliyo safi kwa kuhakikisha mazingira wanatunzwa.
FIFA haijasema chochote kutokana na barua hizo zilizotumwa kwenye makao makuu yake nchini Uswisi Zurich, Rais wa mpira Duniani Giani Infantino amekuwa akisisitiza mara kwa mara lengo kuu lao ni kuleta umoja wa jamii zote kuondoa ubaguzi pamoja na kuhakikisha mpira unachezwa kote Ulimwenguni.
Shirikisho hilo limejikuta likiwa kwenye presha kubwa kwa hivi karibuni kutoka kwa Wachezaji wa kulipwa wakitishia kutokucheza mashindani ya kalbu bingwa ya Dunia ambayo yanatarajiwa kufanyika mwaka 2025.
Chombo hicho kinachoongoza mpira Ulimwenguni kinatuhumiwa kwa kuangalia zaidi pesa bila kujali afya za Wachezaji kwa kuongeza idadi ya michezo bila kuangalia ufinyu wa muda wao wa kupumzika ambapo inasababisha kupata majeraha ya mara kwa mara.