Monday , 21st Oct , 2024

Ni ndani ya Jiji la Dar es Salaam ambapo kelele za utafutaji wa maisha zinashindana na ndoto za walio wengi, hapa ndipo kuna hadithi ya maisha ya Bw. Hamis Omary Uchuro na Bi Hadija ambao ni walemavu wa macho wakazi wa Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.

Safari ya maisha ya wanandoa hawa ilianza tangu mwaka 2007 walipokutana kwenye kongamano la wenye ulemavu wa macho, wanasema licha ya changamoto nyingi  walizokutana nazo kwa kipindi chote cha miaka takribani miaka 17  hadi sasa wana watoto watano wanaowategemea. 

Wamekuwa kivutio zaidi kwa jamii kwa jinsi wanavyokatiza katika mitaa mbalimbali bila kuhitaji msaada wa watu kuwaongoza, wakisema tayari wameielewa vyema mitaa.

"Yaani siku zote mwanzo ni mgumu, wakati ndio tumeona tulihitaji kuelekezwa kila kitu lakini kwa sasa hata wakati wa kuvuka barabara sisi hatuhitaji kusaidiwa" amesema Bw. Hamis Omary. #EastAfricaTV