Levis Mahenge alionekana katika mitandao ya kijamii akimtuhumu Mkuu huyo wa kituo kwa kumpiga hadi kumvunja mkono
Taarifa ya Jeshi la Polisi imesema kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 9/2024 saa 12:30 jioni ambapo baada ya tukio hlo kugundulika na Uongozi wa Polisi Njombe, Jalada lilifunguliwa na ushahidi ukakusanywa na uchunguzi umekamilika
Polisi wamesema hatua za kiinidhamu zinaendelea kukamilishwa dhidi ya mkuu huyo wa Kituo cha Polisi Wilayani Makete na baadaye hatua za kisheria zitafuata kwa sababu tuhuma hizo ni za kijinai