Fred Felix Minziro amejiunga na timu ya Pamba ya Jijini Mwanza baada ya timu hiyo kumfuta kazi Goran Kopunovic. Pamba imeshacheza michezo saba ya ligi kuu Tanzani bara msimu huu wa 2024-2025 mpaka sasa, imetoka sare michezo minne na kupoteza michezo mitatu na inashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 4.
Uongozi wa timu ya Pamba umemuajiri kocha wa zamani wa Kagera Sugar Fred Felix Minziro kuiongoza timu hiyo yenye masikani yake Jiji la Mwanza kuiongoza kwenye pilikapilaka ligi kuu Tanzania bara na kombe la shirikisho la CRDB. Klabu ya Pamba haina muendelezo mzuri katika ligi kuu msimu huu wa 2024-2025 mpaka sasa imeshacheza michezo Saba imefungwa kwenye michezo mitatu na kutoka sare michezo minne.
Wana Tipilindanda ilifanya maamuzi ya kuachana na Wachezaji wake walioipandisha timu daraja pamoja benchi la ufundi na kumuajiri Kocha aliyekua akikinoa kikosi cha Tabora United Goran Kopunovic raia wa Serbia mwanzoni mwa msimu wa 2024-2025, taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zilizotoka siku ya jana zimethibitisha kuachana na kocha huyo aliyewahi kuifundisha klabu ya Wekundu wa Msimbazi baada ya muenendo mbuvu wa kikosi chao kwenye ligi.
Fred Felix Minziro atakuwa na kazi ya kuhakikisha anaitoa timu hiyo kwenye nafasi inayoshika kwa sasa kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara. Pamba ilianza ligi kwa kucheza michezo mingi migumu kutokana na kukutana na timu zenye uzoefu wa ligi pamoja na wachezaji wenye ubora na uzoefu ilicheza dhdi ya Tanzania Prisons, Azam, Singida Big Stars. Kipigo cha goli 4-90 ilichokipata kutoka kwa mabingwa watetezi wa ligi kuu timu ya Wanachi ilihitimisha ajira ya Kopunovic ndani ya Pamba.
Minziro anauzoefu mkubwa wa kufundisha mpira Tanzania kwani alishawahi kufundisha timu mbalimbali za ligi kuu pamoja na ligi ya daraja la kwanza ( Championship ). Baba Isaya ameshawahi kufundisha kwenye vikosi vya Yanga kama kaimu kocha, Tanzania Prisons akiwa kocha mkuu, Kagera Sugar, na Geita Gold FC ambayo aliiwezesha timu hiyo kumaliza nafasi ya nne kwenye ligi msimu wa 2021-2022.
Ligi kuu Tanzania bara itarejea tarehe 18, Oktoba baada ya mapumziko ya kupisha ratiba timu za taifa ambazo zilikuwa zikicheza michezo ya kufuzu mashindano ya AFCON yatakayofanyika 2025 nchini Morocco. Minziro anatarajiwa kukiongoza kikosi cha Wana Kawekamo kwenye mchezo utakaochezwa Oktoba 21,2024 siku ya Jumatatu majira ya saa 10:00 jioni dhidi ya Kagera Sugar.