Wakili Peter madeleka akizungumza na wananchi mbele ya mhakama hii leo
Wakili upande wa mlalamikaji Peter Madeleka akizungumza na waandishi wa habari baada ya maamuzi ya Hakimu Mfawidhi Nyamburi Tungaraja amesema anashangazwa na maamauzi hayo kwani yanalenga kumbeba mlalamikiwa
“Nimeshangazwa na maamuzi haya, iweje mahakama ishindwe kutoa maamuzi ya kukamatwa Kigondo na kupelekwa mahabusu kwa kuidharau mahakama, tutapanda ngazi mahakama kuu.” Peter Madeleka Wakili wa Mlalamikaji
Itakumbukwa kwamba Fatma Kigondo Afande alituhumiwa kuwatuma vijana waliombaka na kumwingilia kinyume na maumbile binti wa Yombo Dovya na wamehukumiwa kufungo cha maisha mara baada ya kukutwa na hatia ya kutenda makosa hayo