Ameyasoma hayo wakati akitoa hotuba fupi mbele ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ibada ya kumbukizi ya miaka 25 ya kifo cha Hayati Julius Kambarage Nyerere kitaifa iliyofanyika jijini Mwanza
“Tusibeze maendeleo tuliyoyapata mpaka leo bila shaka wale wanaoweza kubeza leo waende waka waulize mama zao. Miaka 60 iliyopita maisha hayakuwa kama ya leo hata miaka 50 ninayoifahamu mimi tofauti ipo kuna wakati tuliishi na mimi niliishi musoma kwa muda fulani baada ya vita maisha tuliyokuwa nayo yalikuwa ni maisha magumu ya hovyo na wakati mwingine tuliweza kuvuka ng’ambo kwenda Kenya ili tukanunue mche wa sabuni, tukanunue dawa ya meno hapa kwetu hakukuwa na kitu tulikuwa tunavaa lakini hatufui kwa sabuni na mizizi wale waliokuwepo ilitumika pia kufulia nguo sisi tulienda shule kipande cha sabuni unafulia na kuogea kwa miezi sita alafu unasema hatuja endelea. Kamuulize mama yako atakuadithia jinsi maisha yalivyokuwa.” Amesema Askofu Mkuu Jimbo Katoliki Mwanza Muhashamu Askofu Renatus Ngwande