Monday , 14th Oct , 2024

Lamine Yamal amefunga goli 5 katika michezo 11 msimu huu ndani ya klabu yake ya Barcelona. Mchezo wa El Clasico unatarajiwa kuchezwa Oktoba 27, 2024 katika Uwanja wa Santiago Barnabeu . Yamal ametengeneza safu hatari ya ushambuliaji Barcelona akishirikiana na Robert Lewandoski, Rafinha.

Lamine Yamal amewastua Viongozi pamoja na Mashabiki wa Barcelona kuelekea mchezo wa La Liga dhidi ya Mahasimu Wao Wakubwa Real Madrid (El Clasico). Nyota huyo mwenye umri wa miaka 17 alitolewa nje ya Uwanja akiwa anachechemea kwenye mchezo dhidi ya Denmark muendelezo wa mechi za mashindano ya Mataifa Ulaya.

Lamine Yamal amesababisha hofu na sintofahamu kwenye kambi ya Barcelona baada ya kupata majereha akiwa anaitumikia timu yake ya taifa ya Hispania. Mchezaji huyo Kinda wa maika 17 alionekana akichechemea alipotolewa uwanjani kwenye mchezo dhidi  ya Denmark.

Hofu imekuwa kubwa kwenye kambi ya Blaugrana kutokana na mchezo wa  El Clasico unakaribia na kumkosa mmoja kati ya Mchezaji hatari kwenye safu ya ushambuliaji  Barca ni pengo kubwa . Taarifa kutoka  Shirikisho la Mpira Hispania  (RFEF) zimethibitisha Yamal kurudishwa Barcelona kwa uchunguzi  zaidi na matibabu.

Wachezaji Vijana huwa wanapopata majeraha makubwa mapema husababisha kushuka kwa viwango vyao na kufanya Wengine kushindwa kufikia matarajio ya Wadau wa Mpira Ulimwenguni. Kuna mifano ya Wachezaji Walioaminiwa na timu zao Wakiwa bado wadogo walichezeshwa mechi nyingi bila kupumzishwa kisha kupata majeraha ambayo yalipoteza ramani ya vipaji vyao.

Michael Owen, Ansu Fati, Jack Wilshere, na Abou Diaby Vipaji vikubwa vya mpira wa miguu majeraha yalikatisha muendelezo wa ubora wao sababu ya kutumiwa kwenye michezo mingi mfululizo. Lamine Yamel msimu uliopita wa 2023-2024 alicheza michezo 50 katika mashindano yote inawezekana maumivu ya misuli aliyopata yamesababishwa na uchovu baada ya kucheza bila kupumzika.

Gavi, Pedri pia Wamekosekana kwa vipindi tofauti kwa muda mrefu ndani ya klabu hiyo Mabingwa wa La Liga msimu wa 2022-2023, kupata majeraha ya misuli kwa Lamine Yamal inaweza kuwatonesha kidonda cha Ansu Fati  Mashabiki na Mabosi wa Blaugrana  ambaye alitizamwa kama mmoja wa Mchezaji bora kutoka La Masia lakini anaonekana safari yake imeishia njiani.

Kocha wa Barca Hansi Flick anapaswa kuhakikisha anatengemeza mazingira ya kumpumzisha nyota huyo raia wa Hispania mwenye umri wa miaka 17 ndani ya kikosi chake. Flick raia wa Ujerumani ameweka wazi juu ya umuhimu wa Lamine Yamal ndani ya Barcelona na timu ya Taifa lake la Hispania. Wadau wa Soka wanahofia safari ya Kijana huyo amayetumia mguu wa kushoto ikawa fupi kutokana na kuchezeshwa michezo mingi mfululizo sambamba na kuchezewa rafu nyingi na Wachezaji wa timu pinzani.

Lamine Yamal ndiye Mchezaji bora kwa sasa aliyezalishwa kwenye kituo cha kuzalisha Wachezaji cha La Masia ambacho kimezalisha Nyota wengi kipindi cha nyuma kama Lionel Messi, Andres Iniesta, Xavi Hernandes na Sergio Busquets.