Sunday , 13th Oct , 2024

Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha linamshikilia Jaina Mchomvu kwa tukio la mauaji ya mtoto Mariam Juma (12) mkazi wa kwa Mrombo katika Halmashauri ya jiji la Arusha aliyekutwa ameauwa huku mwili wake ukiwa na majeraha ya kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya shingoni na maeneo mbalimbali

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo

ya mwili wake kisha mwili wake ukifichwa chini ya uvungu wa kitanda kwenye nyumba ya jirani yao.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo, amesema awali mtoto huyo alikuwa ametumwa dukani toka asubuhi lakini hakurejea na ilipofika mchana wazazi wake walianza kumtafuta maeneo mbalimbali baada ya kuingiwa na wasiwasi.

"Hadi sasa tunawashikilia watu watatu akiwepo Jaina Mchomvu mama mwenye nyumba ambaye amekamatwa na Askari Polisi huko Mabogini Moshi, mkoani Kilimanjaro alikokimbilia kujificha baada ya tukio hili kubainika, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Arusha kwa ajili ya uchunguzi zaidi," amesema SACP Masejo

SACP Masejo amesema kuwa Baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa Jaina Mchomvu alihojiwa na kukiri kutenda tukio hilo la mauaji ya mtoto huyo.

Amefafanua kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali za kiuchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo.