Sunday , 13th Oct , 2024

Raia wa Austraalia Skye Nicolson amefanikiwa kutetea ubingwa wake dhidi ya Raia wa Uingereza Raven Chapman kwa pointi katika pambano lililopigwa kwenye uwanja wa Kingdom Arena nchini Saudi Arabia katika Jiji la Riyadh.

Bondia wa Australia amefanikiwa kutetea ubingwa wake wa WBC uzito wa Unyoya baada ya kupata ushindi wa pointi kutoka kwa Majaji walioshuhudia pambano hilo. Pambano la kwanza la ubingwa kwa uapande wa Wanawake kufanyika nchini Saudi Arabia limetizamwa kama ni hatua chanya kwa Taifa hilo kwenye michezo kwa upande wa Wanawake na tunaweza kuanza kushuhudia Mabondia Wakike kutoka Saudi Arabia wakipambana ulingoni.

Bondia kutoka Australia Skye Nicolson amefanikiwa kutetea mkanda wake wa ubingwa wa WBC wa uzito wa Unyoya dhidi ya Raven Chapman siku ya jana Jumamosi Oktoba 12, 2024 nchini Saudi Arabia Jijini Riyadh.

Nicolson amemshinda Mpinzani wake kwa pointi 99-91 na 98-92, ushindi huo unamfanya nyota huyo kufikisha ushidi wake wa 11 katika mapambano 11 tangu aanze kupigana ngumi za kulipwa. Pambano hilo lililoweka histori Saudi Arabia kuwa la kwanza kufanyika nchini humo kwa upande wa Wanawake kugombania ubingwa wa Dunia.

Mwaka 2018 Serikali ya Saudi Arabia ilibadili sheria iliyokataza Wanawake kuendesha vyombo vya moto na kuhudhuria michezo viwanjani imeanza kulegeza baadhi ya sheria kandamizi kwa  kuzuia  Wanawake kujihusisha na maswala ya michezo ikiwemo kuhudhuria viwanjani kwenye michezo mbalimbali.

Pambano la Nicolson dhidi ya Chapman linaweza kuwa ni hatua muhimu kwa taifa hilo la Kiarabu lenye misimamo mikali ya sheria za Kidini kuruhusu Mabondia wa Kike kuanza kupambana ulingoni  sambamba na michezo mingine. 

Mpaka sasa nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta ya Petrol inawakufunzi wawili tu Wanawake katika michezo ya mapigano Rasha Al Khamisi na Halal Alhamrani, kufanyika kwa pambano la ubingwa kwa Wanawake na kushushudiwa na Maelfu ya Mabinti kunaweza kushawishi Wazazi kuruhusu Watoto Zao wenye jinsia ya Kike kuanza kujihusisha na michezo ya ngumi.

Hatua hiyo imepokelewa kwa furaha na Mataifa ya Magharibi na kuipongeza Saudi Arabia kwa kufanya mabadiliko makubwa katika sekta ya michezo kwa Wanawake bila kuathiri tamaduni zao.

Saudi Arabia kwa kipindi cha Miezi 12 iliyopita imeandaa mapambano makubwa ya uzito wa juu yakiwemo yaliyowahusisha Mabondia kama Antony Joshua, Tyson Furry na Francis Ngannou.