Friday , 11th Oct , 2024

Kwenye tukio lililopewa jina la ''WE ROBOT''  Bilionea Elon Musk ametambulisha bidhaa mpya ambazo zimezalishwa na kampuni yake ya Tesla Inc.

 

Kwenye tukio hilo lilofanyika oktoba 10 huko Califormia, moja ya kitu ambacho kilivutia wengi ni roboti ambao wanatambulika kwa jina la ''Optimus'' roboti hawa waligeuka kivutio kikubwa kwa waudhuriaji wa tukio hili kwani walikuwa wakizagaa kama lile ten la Marioo alafu pili na tatu walikuwa wakibeba maboksi ya zawadi na kugawa vinywaji mithili ya wahudumu wa Baa

Mbali na ''optimus'' bidhaa nyingine ambayo ilitambulishwa kwenye macho ya wahudhuriaji ni gari ndogo mfanano wa (Corolla Hybrid) ambayo inatumia mfumo wa akili mnemba kujiendesha yenyewe pasi na kuhitaji dereva hii ilitambulishwa kwa jina la ''Cybercab'' ila kubwa zaidi ni gari mfanano wa Hiace iliyobeba sifa ya kujiendesha yenyewe kwa kutumia akili mnemba na kubeba watu si chini ya 20 na kubatizwa kwa jina la ''Robovan'' 

Optimus kwenye tukio hilo alionekana akifanya kazi za nyumbani kama Atieno vile, ila utofauti wake ni kwamba alikuwa akimwagilia mimea, kubeba mizigo mithili la mpagazi, kwenye video ambayo ilioneshwa kwenye tukio hilo. 

Wakati video hiyo ikiwaonesha Optimus wakifanya majukumu ya nyumbani, Elon Musk alichagiza kwa kusema Optimus pia anaweza kufanya mazoezi na mbwa wako, kulea mtoto wako, kukata majani kwenye bustani na kazi nyinginezo.

Lakini mzozo upo kwenye bei ya roboti huyu ambapo Bilionea Elon alisema ili uweze kummiliki Optimus basi kitahitajika kiasi cha milioni 54 hadi milioni 81 ''nadhani itakuwa ndiyo bidhaa kubwa na ya aina yake kupata kutokea alisema Elon

Lakini kwa yeyote ambaye atakuwa na mahitaji ya Roboti Optimus atahitajika kusubiri kwa miaka miliwi mpaka mwaka 2026 ndipo ataanza kuuzwa rasmi.