Mwanahawa Shomari
Simulizi ya mama huyu aitwaye Mwanahawa Shomari, mkazi wa Tegeta Wazo jijini Dar es Salaam anayesumbuliwa na magonjwa ya Figo, Ini na Moyo ilianza kuwa ngumu tangu mtoto wake wa kiume alipoamua kumtelekeza na sasa anakaa kwa mwanae wa kike ambaye pia hali yake ya maisha si nzuri.
Mama huyu anasimulia kuwa amekosa pesa ya kwenda hospitali kufanyiwa vipimo zaidi na kuanza matibabu, hivyo kuomba watanzania watakaoguswa kumchangia ili apate tumaini la kunyanyuka tena kitandani hapo.
Mawasiliano ya kumpata ama kumtumia chochote ni kupitia namba ya bintiye, 0714842036 jina Amina Mwinshehe.