Jurgen Klopp mwenye umri wa miaka 57 amekubali kurejea kwenye soka lakini kwa kubadili majukumu yake ambapo kocha huyo wa zamani wa vilabu vya Mainz 05,Borrusia Dortmund na Liverpool ataanza kutekeleza majuku yake mapya Januari 1, 2025
Kocha wa zamani wa klabu za Mainz 05, Borrusia Dortmund na Liverpool ameteuliwa na kampuni inayotengeneza vinyaji vya kusisima mwili kampuni ya Red Bull, kusimamia maendeleo ya michezo kwenye timu zote zinazomilikiwa Red Bull.
Klopp raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 57, alitangaza kuachana na majukumu yake ya Ukocha mwishoni mwa msimu wa 2023-2024 baada ya kusema anahitaji kupumzika kutokana na kupoteza nishati ya upambanaji akiwa kama Mwalimu wa soka.
The normal One kama anavyofamika na Mashabiki wa Liverpool, akiwa Borrusia Dortmund alifanikiwa kutwaa Bundesliga 2011-2012,2012-20213, DFB Pokal 2011,2012, DFL SuperCup 2013 na 2014.
Pia aliwawezesha Majogoo ya jiji la Anfield kutwa kombe la EPL 2019-2020, Kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya 2018-2019, pamoja kombe la ligi 2021/2022, 2023/2024, FA Cup 2021/2022, Ngao ya Hisani 2023, Kombe la Dunia la Klabu 2019 na Kombe la UEFA Supa Cup 2019.
Jurgen Klopp anazungumzwa kama mmoja wa Makocha bora wa muda wote wa soka waliowahi kutokea Duniani kutokana na uwezo wake wa kutengeneza timu shindani kwa kutumia bajeti ndogo ya usajili.
Kwenye majukumu yake mapya atafanya kazi ya kushauri timu zote zilizo kwenye chini ya mwamvuli wa kampuni ya Red Bull kuhusiana na Falsafa ya timu, usajili wa wachezaji, maendeleo ya makocha sambamba na maendeleo ya uzalishaji wa Wachezaji wapya.
Red Bull inamiliki timu mataifa tofauti Duniani zikiwemo RB Leipzig Ujerumani, Red Bull Salzburg Austria, New York Red Bull Marekani na Red Bull Bragantino nchini Brazil. Klopp anatarajia kuanza kutekeleza majukumu yake mapya Januari 1, 2025