Monday , 7th Oct , 2024

Simba SC kutoka Tanzania imepangwa kwenye kundi A kombe la shirikisho na timu mbili kutoka ukanda wa Afrika ya kaskazini CS Sfaxien ya Tunisia na CS Constantine ya nchini Algeria, Wekundu wa Msimbazi wanarekodi nzuri dhidi ya timu za Kiarabu je Simba wanaweza kuendeleza rekodi yao?

Simba imepangwa kundi A kombe la shirikisho Afrika sambamba na CS Sfaxien ya Tunisia na CS Constantine ya nchini Algeria

Wawakilishi wa Tanzania katika kombe la shirikisho barani Afrika Simba SC wamepangwa kundi A kwenye droo ya hatua ya makundi iliyofanyika mchana huu makao makuu ya shirikisho la soka Afrika CAF, Cairo nchini Misri.

Simba imepangwa na timu za CS Sfaxienya Tunisia, CS Constantine ya nchini Algeria na FC Bravos do Maquis ya Angola. Wekundu wa Msimbazi si Wageni wa kupangwa katika kundi linaloonekana la kifo katika makaratasi walishawahi kupangwa katika kundi moja na Al Ahyl ya Misri, AS Vita ya Congo DRC na El Merekh ya Sudan,  Simba ilifanikiwa kucheza hatua ya robo fainali kutoka kwenye kundi hilo nyuma ya Al Ahyl.

Kabla ya kuingia kwenye makundi ya kombe la shirikisho katika droo ya siku ya leo Wekundu wa Msimbazi waliiondosha mashindanoni klabu ya Al Ahyl Tripol ya nchi Libya kwa ushindi wa goli 3-1 katika dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam baada ya suluhu ya kutokufungana nchini Libya.

Michezo ya makundi kwa kombe la shirikisho Afrika inatarajiwa kuanza kuchezwa wiki ya mwisho wa mwezi Novemba 2024, Simba inajivunia zaidi uwanja wao wa nyumbani ambao kwa kiasi kikubwa mafanikio yao ya kucheza robo fainali mara 4 kombe la klabu bingwa na mara 1 kombe la shirikisho imetokana na nguvu yao katika uwanja wa nyumbani.