Tuesday , 24th Sep , 2024

Wananchi wa mtaa wa Gaza, uliopo Mwananyamala jijini Dar es Salaam, wameiomba Serikali iwasaidie kupata haki ya kijana wa mtaa huo aitwaye Ijumaa Juma (22) ambae amefungwa Jela miaka 30 kwa kosa la kubaka binti wa miaka 14.

Wananchi waomba msaada waweze kukata rufaa

Akiongea kwa uchungu mama wa kijana huyo Asia Rashid, anasema mzazi wa binti aliyebakwa huwa anatumia fedha zake akitaka kumuondoa mtu yeyote anatuMia fedha zake kuwaumiza wa hali ya chini.
"Wanasema mwanangu alibaka hapa uwanjani kwa mnavyoona hapa mtu akibakwa watu hawatoona, tazama uwanja huu ulivyozungukwa na nyumba ubakaji gani unaoweza kufanyika katika uwanja huu, tunaomba Serikali yetu itusaidie kupata haki ya mtoto wetu kwa maana amefungwa miaka 30 jela", alisema Asia Rashid, Mama wa kijana aliyefungwa.

Majirani wanamzungumziaje Ijumaa Juma aliehukumiwa miaka 30 jela?
"Mimi mjukuu wangu kakma unavyoniona niko na macho yangu mpaka yanapofuka huyu kijana hana shida na aliyemsingizia tunamjua aliwahi kutembea na mtoto wa dada yake akampa ujauzito halafu akamwambia yule mtoto asema mimba ni ya Ijumaa badae akaitoa, kwahiyo huyu baba ni tabia yake", alisema Rukia Rashid, Jirani.

"Tunaomba msaada kuanzia ngazi ya mtaa, kata, wilaya, mkoa mpaka taifa , kwa mazingira ya kesi hii sisi masikini hatuwezi kumsaidia huyu kijana tunachangishana kila siku fedha kwa ajili ya kutafuta wakili lakini peke yetu hatuwezi tunaomba msaada wa Serikali wamsaidie huyu kijana amekatuza ndoto zake", alisema  Zuhura Mohammed, Jirani.
"Dada kama unavyoona hapa ndio uwanjani na hapa ndio wanasema amebaka na huu uwanja kila siku tunafanya mazoezi hapa dada mtu anabakwaje mtu mwingine asione rafiki yetu amefungwa tuna maumivu tunaomba Serikali ya mama samia imsaidie aweze kupata haki yake", alisema Ally Sunny, Rafiki wa mfungwa.

Sheria inasemaje kuhusu wananchi kutokubaliana na hukumu za kesi?
"Kama mwananchi hajakubaliana na hukumu sasa hapo inategemea kama Kesi ilikuwa ngazi ya kata inabidi ikatiwe rufaa ngazi ya wilaya, na kama ilikuwa Mahakama kuu inabidi ipelekwe rufaa na baada ya hapo anaweza kupata haki yake na Mahakama ya rufaa ikitoa hukumu wasiporidhishwa pia wanawea wakakata rufaa pi", alisema Wakili William Maduhu-Afisa uchechemuzi LHRC.

Aidha Wakili Maduhu anaelezea sehemu ya wananchi kupata msaada wa kisheria
"Kuna vituo na mashirika mengi ya kutoa msaada wa kisheria hasa kwa wananchi ambao hawajiwezi kiuchumi, mashirika hayo ni pamoja na LHRC, TLS, TAWLA, WILDAF , TANLAP, kama mwananchi hana uwezo wa kuweka wakili anaweza kwenda kwenye hayo mashirika" ,  alisema Wakili William Maduhu-Afisa uchechemuzi LHRC.