Monday , 23rd Sep , 2024

Bondia wa Uingereza Daniel Dubois anasherehekea ushindi wake wa masumbwi uzito wa juu IBF, dhidi ya Anthony Joshua katika Uwanja wa Wembley Jumamosi, Septemba 21,2024. Mchezo uliomalizika kwa Joshua kupigwa kwa K.O raundi ya tano ya mchezo.

Daniel Dubois  sasa anahitaji kulipiza kisasi kwa bondia Oleksandr Usyk, ambaye alimpiga Dubois kwa TKO mnamo Agosti 2023. Dubois anahitaji pambano na Bingwa huyo wa Ukraine ili kucheza  pambano la ubingwa wa dunia ambalo litamuweka katika nafasi nzuri ya uzito wa juu.

Promota Frank Warren ameeleza changamoto ya kupanga pambano na Tyson Fury, akisisitiza  kuwa kuna  "ugumu sana" Hata hivyo, Dubois amebaki na mtazamo wa kutaka kukutana na Usyk, akionyesha hamu kubwa ya kurekebisha makosa ya zamani na kudhihirisha ubora wake katika mchezo ngumi.