Friday , 20th Sep , 2024

Serikali imesema haitawavumilia watumishi wa umma wenye kasumba ya kufanya kazi kwa mazoea hali inayopelekea malalamiko kutoka kwa wananchi kwa kushindwa kupata huduma bora 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deus Sangu

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deus Sangu, ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha watumishi wa Manispaa ya Tabora mara baada kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi, ikiwa ni ziara ya kimkakati ya kuwafuata watumishi katika maeneo yao ya kazi  badala ya kuja Dodoma

Amesema tabia hiyo imekuwa ikikwamisha azma ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuona wananchi wanahudumiwa ipasavyo katika ofisi za serikali

Amewataka watumishi hao kutambua kuwa suala la  kutoa huduma bora kwa wananchi si hisani bali ni wajibu 

Katika hatua nyingine Mhe. Sangu amezitaka mamlaka za ajira na nidhamu kusimamia haki na stahiki zote za watumishi huku akizionya mamlaka hizo kushauri ipasavyo bila kuwaumiza watumishi kwa lengo la kuwafurahisha viongozi wao.

Amesema ni jambo la aibu kuona watumishi wakiwasilisha changamoto zao  mbele ya Viongozi wa Kitaifa wanapofanya ziara katika maeneo yao ilihali changamoto hizo zingetafutiwa ufumbuzi katika ngazi ya wilaya au mkoa.