Wednesday , 18th Sep , 2024

Baada ya kukumbana na purukushani za muda mrefu ni rasmi sasa instagram wameamua kunyoosha mikono juu na kusalimu amri

 

Instagram kwa sasa wametambulisha Teen Accounts, Account ambayo imelenga kumlinda mtumiaji wa mtandao huo aliye kwenye kundi la umri chini ya miaka 16.

Teen accounts inakuja na ulinzi mkubwa ndani yake kwa vijana wanaotumia mtandao huo, ikiwemo aina ya maudhui ambayo wanaweza kuyaona, watu ambao wanaweza kuchangamana nao (interact) na kuzuiwa kuona maudhui yaliyobeba mambo yasiyofaa kwa kijana.

''Leo tumetatmbulisha teen accounts kwenye mtandao wa instagram, ikiwa na maana kwamba mtu yeyote aliye na umri chini ya miaka 16 kwenye mtandao wa instagram atawekwa kwenye kizuizi maalumu ambacho kikofaragha moja kwa moja (Private by default) 

Ni kwa miaka sasa mitandao ya kijamii imekuwa ikikosolewa kwa kile kinachotajwa kwamba wameshindwa kuwalinda watoto dhidi ya maudhui yanayopatikana kwenye mitandao yao, sheria zimekuwa zikiwabana kwa kosa hilo. Lakini kwa sasa Instagram wametambulisha Teens accounts kufanya mtandao huu kuwa salama zaidi kwa watoto wanapotumia

Kwa hiyo kwanza kabisa accounts za watoto zitazuiwa moja kwa moja na pia hakuna mtu ambaye ataweza kutuma ujumbe kwenye account ambayo inamilikiwa na mtoto (DM). kitu kizuri zaidi kuhusiana na hii imewagawa watoto kwenye makundi mawili wale walio na umri chini ya miaka 16 na wale ambao wako na umri juu ya miaka 16, Lakini hawa ambao wako na umri chini ya miaka 16 vizuizi kwao viko kwa ukubwa zaidi kiasi kwamba mzazi wake ndiye anayehitajika kutembelea account ya mtoto kufahamu kile ambacho anakifanya kwenye mtandao wa Instagram'' alisema Barbar Ortutay mwandishi wa habari za teknolojia kutoka AP news

Kwa maana hiyo mtumiaji wa mtandao wa Instagram aliyepo kwenye kundi la umri wa miaka 16 kushuka chini, atajikuta kwenye kundi hili la Teens accounts apende asipende.