Wednesday , 18th Sep , 2024

Zaidi ya makocha kumi wametuma CV katika klabu ya Kengold wakihitaji Kwenda kufundisha klabuni hapo baada ya Fikir Elias kutangaza kuachia ngazi ndani ya kikosi hiko kinachoshiriki ligi kuu ya NBC kwa mara ya kwanza.

Katika makocha hao makocha 6 wameshawahi kufundisha katika ligi hii akiwemo kocha wa zamani wa Coastal Union na wekundu wa msimbazi Simba Juma Ramadhani Mgunda, Zuberi Katwila, Fransis Baraza, Malale Hamsini na Mburundi Haruna Hermana

Kengold inashika nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi kuu baada ya kucheza mechi 3 pasi na ushindi wowote.