Friday , 13th Mar , 2015

Serikali ya Tanzania leo imetiliana saini ya Mkopo wa Shilingi Billion710 toka Benki ya Dunia kwa ajili ya miradi mitatu mikubwa ya Maendeleo hapa nchini.

Makao makuu ya benki ya Dunia.

Akipokea Msaada huo kwa niaba ya Serikali Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Servacius Likwelile amesema kati ya Fedha hizo Bilion 537.9 zitatumika kuboresha jiji la Dar es salaam ikiwa ni pamoja na miundombinu na Utawala,.

Billion107 zitatumika kwa ajili ya Mikopo ya nyumba za garama nafuu ambazo zitakopeshwa kwa Taasisi za mikopo huku Bilion64.5 zenyewe zimeelekezwa katika Uvuvi.

Likwelile amewataka Watendaji wote ambao Fedha hizo zitapelekwa wawe waaminifu na kuzitumia kwa Malengo mahususi na kukemea vitendo vyovyote vya Ubadirifu na Ufisadi wa fedha hizo za Mkopo..